Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

Emery anataka point za chelsea

Emery amewaambia mastaa wake anachohitaji ni kushinda mechi hiyo ya pili baada ya ile ya kwanza kuchapwa na Manchester City kwenye uwanj...


Image result for emery arsenal
Emery amewaambia mastaa wake anachohitaji ni kushinda mechi hiyo ya pili baada ya ile ya kwanza kuchapwa na Manchester City kwenye uwanja wa nyumbani wa Emirates.
Kwenye mazoezi hayo, Emery alionekana kufanyia kazi zaidi safu ya ushambuliaji akimwonyesha straika wake Pierre-Emerick Aubameyang namna ya kufanya kuleta ushindi kwenye mechi hiyo ya Chelsea itakayofanyika uwanjani Stamford Bridge.
Aubameyang, ambaye alitua Arsenal kwenye dirisha la Januari akitokea Borussia Dortmund alifunga mabao 10 katika mechi 13 alizoitumikia Gunners kwa msimu uliopita.
Mesut Ozil na mastaa wengine kibao akiwamo kiungo, Lucas Torreira walionekana wakishiriki vizuri kwenye mazoezi hayo na hivyo kinachosubiriwa ni hiyo kesho kufika kuna kama kutakuwa na manufaa ya ndani ya uwanja.
Emery alisema: “Kila mechi ni tofauti. Tunataka kujiandaa kwa kila mechi kutokana na mpinzani alivyo. Tunachohitaji ni kwenda kushinda mechi hiyo dhidi ya Chelsea.”

No comments