Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

Barca yamweka kiporo Pogba

Barcelona wameripotiwa kwamba wamemweka kiporo kiungo wa Manchester United, Paul Pogba na kwamba watamfungia kazi ya kumsajili kwenye ...


Barcelona wameripotiwa kwamba wamemweka kiporo kiungo wa Manchester United, Paul Pogba na kwamba watamfungia kazi ya kumsajili kwenye dirisha la majira ya kiangazi la mwakani.
Kwenye orodha ya wachezaji wengine inaowasaka Barcelona ambao imesema itawafanyia kazi mwakani ni staa wa PSG, Adrien Rabiot na kinda wa Ajax, Frenkie de Jong
Mabingwa hao wa La Liga walihusishwa na mpango wa kumsajili Pogba katika dirisha hili la majira ya kiangazi, lakini Man United wameripotiwa kugoma kumwaachia aondoke licha ya kupewa ofa ya Pauni 45 milioni pamoja na wachezaji Yerry Mina na Andre Gomes kwenye dili hilo ili tu Mfaransa huyo aende Nou Camp.
Kuhusu wachezaji wengine, Rabiot amekuwa mtu muhimu kwenye kikosi cha kocha Thomas Tuchel huko PSG, huku De Jong akifanya mambo makubwa akiwa na timu ya Ajax. Taarifa zinadai kwamba Barcelona itasajili wachezaji wawili kwenye orodha hiyo ili kuboresha safu yao ya kiungo kwenye dirisha la uhamisho wa majira ya kiangazi la mwakani

No comments