Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

KAMA UNADHANI YANGA WANA HOFU NA WAARABU SAHAU KABISA

Baada ya kutoa dozi za maana mkoani Morogoro ikiwemo ile ya 5-1 dhidi ya Tanzanite Academy, uongozi wa Yanga umesema hauna hofu na waar...


Baada ya kutoa dozi za maana mkoani Morogoro ikiwemo ile ya 5-1 dhidi ya Tanzanite Academy, uongozi wa Yanga umesema hauna hofu na waarabu hata kidogo.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa klabu, Dismas Ten, amesema kuwa Kocha Mkuu wa kikosi, Mkongomani Mwinyi Zahera ameeleza kuiamini timu yake baada ya kucheza mechi nne za kirafiki.

Zahera ameonekana kukoshwa na kiwango cha timu yake baada ya kushinda mechi zote mkoani Morogoro ambazo Yanga ilicheza ikizitumia kwa ajili ya maandalizi ya kukipiga na USM Alger Jumapili ya wiki hii.

Yanga watashuka dimbani kucheza na Alger ukiwa ni mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika ambapo utakuwa ni wa mkondo wa pili.

Kuelekea mechi hiyo, Yanga wamesema watapambana kwa namna yoyote ile ili kuwamaliza Waarabu ili waweze kuweka heshima.

Katika kundi D ambalo Yanga ipo, mpaka sasa imeshikilia mkia ikiwa na alama moja pekee huku Gor Mahia FC yenye alama 8 ikiwa nafasi ya kwanza ikiwaacha USM Alger walio nafasi ya pili kwa tofauti ya mabao ya kufungwa na kufunga na Rayon Sports ikishika namba 3 na alama 3.

No comments